Writen by
sadataley
11:22 AM
-
0
Comments
Kwaya ya Tumaini kutoka kanisa Anglikana Mtakatifu James Kaloleni jijini Arusha imeendelea kujidhatiti katika suala zima la kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji baada ya kufanikiwa kununua basi la pili la kusafiria aina ya Double Coaster huku wakitarajia kuweka wakfu kanda yao mpya ya sauti siku ya jumapili ijayo ya tarehe 8 kanisani kwao Kaloleni.
Kwaya hiyo ambayo inamiliki vyombo vya kisasa vya muziki, ilifanikiwa kununua basi miaka ya karibuni na sasa limefanikiwa kuongeza gari hilo la pili hali ambayo inaonyesha malengo waliyojiwekea kama kwaya yanaendelea kutimia. Kwa upande wa kanda mpya ambayo wanatarajia kuizindua jumapili hii wameipa jina la "Nisamehe" ikiwa na jumla ya nyimbo 10 zenye mahadhi tofauti, ambapo kuelekea tukio hilo, hapo jana waumini wa kanisa hilo waliweza kupata wasaa kwakusikiliza nyimbo hizo.
![]() |
Mabasi ya kwaya ya Tumaini yakiwa yameegeshwa eneo la kanisa St.James. |
![]() |
Wanakwaya na waumini wa kanisa la St.James wakifuatilia ujio wa album mpya ya Tumaini wakati wa ibada jana. Habari na Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment