Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 24, 2013

Vijana weusi wa Marekani waingiwa uoga

Mama wa Trayvon Martin, kijana Mmarekani mweusi aliyeuliwa Florida mwaka jana wakati akielekea nyumbani, anasema kufutwa kwa kesi ya mwanamgambo wa kulinda mitaa aliyemuuwa kumewafanya vijana wengi weusi wa Marekani kuwa waoga.
Sabrina Fulton, mama wa Trayvon Martin
Akizungumza na BBC, Sabrina Fulton, alitoa wito sheria inayoruhusu kutumia nguvu ya kuweza kuuwa iwapo maisha yako yako hatarini - anataka ibadilishwe katika jimbo la Florida na kwengineko Marekani.
Bi Fulton amepangwa kuhutubia maandamano yanayofanywa mjini Washington kuadhimisha miaka 50 tangu maandamano maarufu yaliyofanywa mjini humo kudai haki za watu weusi na ambayo yaliongozwa na kuhutubiwa na Martin Luther King.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment