Writen by
sadataley
10:06 AM
-
0
Comments
Na Mch. Josephat Gwajima
Mara nyingi Mungu huongea nasi kupitia ndoto kwasababu kwa njia hiyo aliongea na Ibrahimu, Yakobo, Isaka, Farao, Gideoni, Yusufu babaye Yesu, Mariamu na wengine wengi; Mungu hutumia ndoto kuongea na watu sana na kwasababu ya kutokujua wengi wamejikuta wakidharau ndoto.
Hatari ya ndoto huja pale, mtu anapopokea taarifa ya hatari ijayo alafu kwa kupuuzia akashindwa kuishughulikia na matokeo yake jambo hilo likaja likatokea. Ndoto ni taarifa ya ulimwengu wa roho, na ndio maana unapoota ndoto mbaya inabidi uiangamize kabla haijatimia ili lisijekudhihirika katika ulimwengu wa mwili.
Ikitokea umeota ndoto, jambo la kwanza ni kubaini kuwa hiyo ndoto ni nzuri au ni mbaya; kama ndoto ni mbaya unatakiwa mara baada ya kuamka unatakiwa uivunje katika jina la Yesu Kristo kulingana na ndoto uotayo.
Na ikitokea umeota ndoto nzuri, basi iamuru itimie katika jina la Yesu, ukiamka unasema katika jina la Yesu ninaomba ndoto niliyoota itokee katika jina la Yesu.
Ikitokea umemuota mtu mwingine ndotoni ujue Mungu amekuonyesha ili uishughulikie, na si lazima umwambie yule uliyemuota kwasababu Mungu amekuonyesha wewe ili uishughulikie.
Habari na Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment