Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 20, 2013

Rais Kenyatta azuru China

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa China Xi Jinping  August 19, 2013
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa China Xi Jinping August 19, 2013
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikutana na rais wa China Xi Jinping  Jumatatu katika ziara rasmi mjini  Beijing, inayolenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi zao mbili. Wachambuzi wa maswala ya kisiasa hata hivyo wanasema  huenda pia  rais Kenyatta anatafuta rafiki mwenye ushawishi mkubwa kudhoofisha kesi ya mahakama ya kimataifa – ICC dhidi yake.

Bw. Kenyatta  alikaribishwa rasmi na kwa taaadhima kuu na mwenyeji wake rais Jinping akiwa pamoja na wafanya biashara wa Kenya. Ziara hiyo inalenga kujenga mahusiano  ya kiuchumi na China na kutafutia bidhaa za Kenya soko nchini humo.
 
Rais huyo wa Kenya alielezea manufaa ya ushirika wa China na Kenya, akitaja maendeleo na uwekezaji ambao umeimarisha miundombinu nchini mwake hususan barabara.
 Bw. Kenyatta alikwenda China baada ya kukutana na maafisa wa Russia mjini Moscow ambapo pia alishuhudia wanariadha wa Kenya wakishindana katika mbio za masafa marefu na kujishindia medali kadhaa za dhahabu.

China na Russia ni wanachama wa kudumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ni maarufu kwa kutumia kura ya turufu kupinga miswada yoyote yenye utata wa kisiasa. Maafisa wa Kenya na wale wa Umoja wa Afrika wamekuwa wakiliomba baraza hilo la Umoja wa Mataifa  kuiomba mahakama ya kimataifa ICC kurejesha nchini Kenya kesi za uhalifu wa kivita dhidi ya rais Kenyatta na wakenya wengine.

Mchambuzi wa maswala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Nairobi Adams Oloo aliiambia Sauti ya Amerika kuwa ziara ya rais Kenyatta inatoa ujumbe wazi  kuwa Kenya inatafuta washirika wenye nguvu  na kwamba haitegemei  msaada wake kutoka nchi za Magharibi pekee.

Imewekwa na Happy Adam 


« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment