Writen by
sadataley
12 years ago
-
0
Comments
Na Pamela Mollel, Simanjiro
SERIKALI kupitia Idara ya Madini, Kanda ya Kaskazini imefungua migodi minne iliyopo kitalu D katika migodi ya madini ya Tanzanite Mererani,wilayani Simanjiro mkoani Manyara iliyokuwa imefungwa baada ya kutokea mauaji ya mchimbaji yaliyotokea hivi karibuni.
Akithibitisha kufunguliwa kwa mgodi huo Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Benjamin Mchwampaka, alisema baada ya uchunguzi kukamilika waliamua kuufungua ili wachimbaji waweze kuendelea na shughuli za uchimbaji.
"Tumefungua migodi hiyo ili kupisha shughuli za uchimbaji kuendelea na pia tunasisitiza kila mgodi uchimbe eneo lake bila kuingilia mwingine ili kuepusha migogoro ya kila siku," alisema," Mchwampaka
No comments
Post a Comment