Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, August 21, 2013

Kenya na China zatiliana saini mkataba wa uchumi

Rais wa kenya Uhuru Kenyatta (L) na Rais Xi Jinping wa China
Rais wa kenya Uhuru Kenyatta (L) na Rais Xi Jinping wa China
Serikali ya Kenya imetiliana saini na serikali ya China mikataba yenye thamani ya dola bilioni tano kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa reli, nishati na ulinzi wa wanyamapori.

Mkataba huo ulitiwa saini wakati wa ziara ya kwanza ya Rais Uhuru Kenyatta huko China tangu aliposhinda uchaguzi wa mwezi Machi mwaka huu.

Rais wa China Xi Jinping  alisema wakati wa sherehe za kutia saini kwamba Bwana Kenyatta ataweza kuiongoza Kenya kuelekea uchumi uliokamilika.

Uhusiano wa kiongozi huyo wa Kenya na nchi za magharibi unaweza ukakumbwa na matatizo kutokana na hali kwamba anakabiliwa na mashtaka huko The Hague yanayohusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Seneta Murkomen Kipchumba  wa Kenya amesema mkatabu huo ni muhimu sio tu kwa Kenya bali kwa nchi za Afrika Mashariki.

Anasema mpango wa ujenzi wa njia ya reli utasaidia sana nchi za Afrika ya kati kupanuka kiuchumi na kupunguza sana msongamano wa bidhaa kwenye bandari ya Mombasa.

Imewekwa na Happy Adam

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment