UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Sunday, August 18, 2013

Kamati ya Bunge yapokewa kwa mabango Machinga Complex

Majengo maalumu kwa ajili ya shughuli za wafanya biahsara wadogowadogo maarufu kama Machinga Complex yaliyopo jijini Dar es Salaam 
Na Kalunde Jamal, Mwananchi 
Dar es Salaam. Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, mwishoni mwa wiki ilipokewa kwa mabango na kufungiwa milango ilipotembelea Soko la Wafanyabiashara ndogondogo la Machinga Complex na Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (Uuda), kwa ajili ya kukagua shughuli zinazofanyika katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamisi Kigwangalla, ilibidi afanye kazi ya ziada kuwasikiliza Machinga hao waliokuwa wakitaka bodi ivunjwe kwa madai ya kutotendewa haki na mwenyekiti wake, huku wakitaka Meneja wa jengo hilo, Nyamsukura Masondole, aendelee kuwawakilisha kwa kuwa anawasikiliza.
Akizungumza na Kamati za Bunge kwa niaba ya wenzake, Makamu Mwenyekiti wa Machinga, Jerard Mpagana, alisema anashangaa hata kumwona Meya wa Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi, kwa sababu hana utaratibu wa kuwatembelea licha ya matatizo lukuki.
Kigingi kingine kilikuwa Uda, baada ya kufungiwa milango na walinzi waliokuwapo getini.
bila kujali kama lililotangulia mbele ni gari la Meya wa Jiji likiwa na nembo ya jiji.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment