Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, August 3, 2013

ILANI YATOLEWA KUHUSU MAZIWA NEW ZEALAND

Serikali ya New Zealand imeonya kwamba maziwa pamoja na maziwa ya watoto wachanga kutoka kampuni moja maarufu, huenda yana bacteria wanaosababisha kupoooza, bacteria wa botulism.
                              N'gombe wakikamuliwa maziwa, Darfield, New Zealand
Uchina tayari imetaka bidhaa hizo zirudishwe na kuagiza bidhaa zote zinazoingia nchini humo kutoka New Zealand zikaguliwe.
Kampuni kubwa ya maziwa ya Fonterra imesema imewaarifu wateja wake katika nchi kadhaa pamoja na Australia, Thailand, Malaysia, Vitenam na Saudi Arabia dhidi ya kutumia bidhaa hizo.
Inafikiriwa bacteria hao wanatoka kwenye mabomba ambayo hayakusafishwa sawa-sawa.
Gary Romano, ni mkuu wa kampuni ya Fonterra nchini New Zealand na amesema kampuni yake inajitahidi kudhibiti tatizo hilo:
"Tuna wasi-wasi sana sana juu ya afya ya binaadamu, na tunafanya kila tuwezalo kuzuwia bidhaa zisifikie wateja.
Mimi nataka kuzungumza juu ya watu, siyo kampuni.
"

Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment