Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Florida kati ya tarehe 17 hadi 20 mwezi huu kujadili masuala ya biashara, mpango wa kinyuklia na makombora wa Korea Kaskazini na suala la raia wa Japan wanaoshikiliwa mateka na Korea Kaskazini kwa miongo kadhaa sasa.
Abe anapanga kukutana na Trump kabla ya kiongozi huyo wa Marekani kufanya mkutano wa kihistoria na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwishoni mwa mwezi Mei.
Abe amesema wanahitaji kuendelea na shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ili ichukue hatua madhubuti kuachana na mpango wake wa kinyuklia katika rasi ya Korea.
Mwezi uliopita, Trump aliongeza ushuru dhidi ya bidhaa za bati na chuma zinazoingizwa Marekani kutoka nje ambapo Japan ni miongoni mwa nchi zinazoathirika na ongezeko hilo la ushuru.
No comments
Post a Comment