Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 24, 2014

PICHA ZA IBADA YA KUSIMIKWA MCHUNGAJI KANISA LA KILUTHERI JIJINI LONDON


Askofu Martin Lind akizungumza jambo.
Siku ya jumamosi mchana kumefanyika ibada kubwa ya kusimikwa kwa mchungaji Moses Shango wa kanisa la Kilutheri usharika wa mtakatifu Anne's jijini London ukiongozwa na askofu mkuu wa kanisa hilo nchini Uingereza Martin Lind.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe, mkewe, wachungaji mbalimbali, waumini pamoja na mchungaji kiongozi wa usharika huo wa Tumaini Kallaghe. Ambapo baada ya ibada hiyo ya kusimikwa kwa mchungaji Moses, waumini walimpongeza kwa zawadi mbalimbali ikiwemo komputa mpakato na kufuatiwa na chakula cha pamoja.

Kanisa la Kilutheri la mtakatifu Anne's huwa na ibada ya kiswahili kila jumapili ya mwanzo na ya kati ya mwezi kuanzia saa nane mchana zikiongozwa na mchungaji kiongozi Tumaini Kallaghe akisaidiwa na mchungaji Moses Shango ambaye amesimikwa rasmi siku ya jumamosi.

Mchungaji Moses Shango akiwa tayari kuingizwa kazini.
Baadhi ya wachungaji na waumini wakifuatilia ibada.
Ibada ya kumsimika ikiendelea.
Maombi yalifanyika.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe na mkewe wakifuatilia ibada.
Waumini wakifuatilia ibada.


Mtume Matthew Jutta na watenda kazi wengine wakiwa ibadani hapo.



Hakika ibada ilipendeza kama inavyoonekana.

Bwana Andy Kilo Mkwavi akiwa ibadani.

Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment