Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, December 18, 2013

Madaktari wauawa kwa shambulio Somalia

Madktari raia wa Syria na wa jamii ya kisomali wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kufanyika shambulizi karibu na mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Moja ya majeruhi katika mlipuko uliotokea nchini Somalia
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia BBC kuwa watu wenye silaha walishambulia gari lililokua likielekea katika hospitali moja.
Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabaab wamekuwa wakisabisha hali ya usalama kuzorota nchini Somalia, hata hivyo haijathibitika ni nani anayehusika na shambulio hilo.Walinzi wao wawili pia waliuawa katika shambulio hilo, huku daktari mmoja wa Syria na mwingine wa Somalia walijeruhiwa .
Madaktari wa Syria wanaelezwa kuwa walikua nchini Somalia kwa ajili ya shughuli za kutoa misaada.
Mwandishi wa BBC ameripoti kuwa shambulio hilo lilitokea katika wilaya ya Siinka Dheer inayodhibitiwa na Serikali, eneo lililo kusini mwa Mogadishu.
Madaktari waliojeruhiwa wako hospitalini wakipatiwa matibabu mjini Mogadishu, halikadhalika miili ya Watu sita waliouawa katika shambulio hilo wamefikishwa hospitalini.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment