Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, December 27, 2013

KRISMASI NDANI YA MITAA YA JIJI LA LONDON, MAFURIKO KUSINI MWA ENGLAND

Hizi ni baadhi ya picha kutoka baadhi ya mitaa ya jiji la London nchini Uingereza jinsi kulivyo wakati huu wa sikukuu ya Krismasi, ambayo hali ya hewa kwa jiji hilo ilikuwa shwari tofauti na baadhi ya sehemu kusini mwa nchi hiyo ambako krismasi haikuwa njema kutokana na mafuriko yaliyosababisha nyumba zao kujaa maji. Angalia picha kutoka London pamoja na kusini mwa nchi hiyo mafuriko yalivyoharibu krismasi kwao.




Picha hizi ni eneo la Covent Garden.


Mitaa ya Leicester square ikiwa imependeza, sehemu hii ni maarufu kwa  uzinduzi wa filamu nyingi maarufu za Uingereza waigizaji huja kuzindulia katika moja ya majengo ya sinema yaliyozunguka enero hili.
Mti wa krismasi ndani ya stesheni ya treni za chini na juu cha Charing cross.
Mti wa Krimasi ambao hutolewa kama zawadi na serikali ya Norway kwa Uingereza kila mwaka, ukiwa unapendezesha eneo la Trafalgar square.
Ibada ikiwa ndio inaelekea kuanza kama projector ikionyesha picha mbalimbali ni ndani ya kanisa la Hillsong London ambao ibada zao hufanyia ndani ya ukumbi wa Dominion theatre.
Mti wa krismasi katika chumba cha watoto wa shule ya jumapili kanisa la St.Barnabas Kensington 
Picha hii ni kutoka mitaa ya Harrow on hill
Hii ni mitaa ya York mambo yalivyokuwa yakionekana ©BBC
Nyumba zikiwa zimezingirwa kwa mafuriko kusini mwa England mapema jana©BBC
Maji yakiwa yamepiga kambi ©thegurdian
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment