Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, November 28, 2013

Mazungumzo ya amani Maziwa Makuu

Marais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila wa DRC (kulia)
Marais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila wa DRC (kulia)
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kwa nchi za Maziwa Makuu  Mary Robinson ,yuko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Alhamis, baada ya kufanya mazungumzo  na maafisa wa Rwanda.
 
 Ziara yake inalenga  kuhamasisha amani katika eneo hilo. Mjumbe huyo maalumu anatarajiwa kuanza ratiba ya mikutano leo mjini  Kinshasa na maafisa waandamizi wa DRC, wabunge na jumuiya za kiraia na baadaye  kutembelea  mji wa Goma mashariki mwa nchi.
 
Kabla ya kuwasili kwake huko Kinshasa mwakilishi huyo maalumu alitembelea Brazzaville, ambako alikutana na rais Denis Sassou Nguesso.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment