Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, April 13, 2018

Shambulio la Marekani Syria litazBalozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa shambulio lolote la anga litakalosababishwa na Marekani nchini Syria litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa "hatuwezi kuepuka uwezekano wowote".ua vita vikali dhidi yetu

Syria Chemical

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMawaziri wakiondoka katika mkutano wa kuijadili Syria ,uliodumu kwa zaidi ya saa mbili
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, ameonya kuwa shambulio lolote la anga litakalosababishwa na Marekani nchini Syria litasabaisha kulipuka kwa vita baina ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa "hatuwezi kuepuka uwezekano wowote".
Bwana Nebenzia ameituhumu Marekani na washirika wake kwa kuiweka amani ya mataifa katika hati hati kwa kile alichokiita "sera za ukatili" na kuelezea hali ya sasa ilivyo kuwa ni ya hatari kupita kiasi.
Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa mataifa ya Ufaransa na Uingereza saa kadhaa zijazo kujadili juu ya kutoa kauli ya pamoja kwa kile wanachoamini utumizi wa sialaha za kemikali uliofanywa na Syria kwenye maeneo ya kitalii yanayoshikiliwa na waasi.Ikulu ya Marekani imearifu kwamba mpaka sasa hakuna kauli ya mwisho iliyokwisha fikiwa juu ya hatua za kijeshi zinazoweza kufikiwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imesema baraza la mawaziri limekubaliana kwamba matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria haipaswi kwenda kinyume lakini hakutoa maelezo ya hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa.
Baada ya mkutano wa dharula uliochukua saa mbili mjini London, taarifa isiyorasmi unasema kwamba Theresa May ataendelea kushirikiana kikazi na nchi za Marekani na Ufaransa ili kuratibu mwitikio wa kimataifa.
Wabunge kutoka Chama cha upinzani cha Labour pamoja na Chama cha Usimamizi wa kihafidhina wametaka kura ya turufu ipigwe bungeni kabla ya majeshi ya Uingereza kuchukua dhamana.

BBC

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment