Writen by
sadataley
7 years ago
-
0
Comments
Kama kawaida ya kila mwezi, Baba Mtakatifu Francisko kutoa ujumbe kwa njia ya Video, hata kwa mwezi Aprili 2018, nia ya maombi yake ya kitume imewaendea wahusika wote katika masuala ya kiuchumi.
Kwa maana hiyo, katika ujumbe wa mwezi wa nne kwa njia ya Video, Papa Francisko anasema kwamba, uchumi hauwezi kutegemea kuongezeka kwa ushuru na kupunguza masoko ya ajira, yanayosababisha kuunda aina nyingi za ubaguzi mpya. Ni lazima kufuata njia ya wafanya kazi, wanasiasa, watafiti na wadau wote wa kijamii ili wawe mstari wa mbele kama binadamu na kufanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha kwamba zinapatikana fursa za ajira yenye hadhi!
Akihitimisha maombi yake kwa njia ya video, Papa anawaalika watu wote kupaza sauti zao kwa pamoja, ili wahusika wa mawazo ya ubunifu na wanao jikita katika masuala ya kiuchumi, wawe na ujasiri wa kukataa uchumi wa kupendelea na kubagua na kwa njia hiyo waweze kutambua namna ya kufungua njia mpya.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
!
Vatican News
!
No comments
Post a Comment