Mtaalam wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Georgia kuweka kipaumbele cha mkakati wa kuwajumuisha wazee na pia kuzingatia usawa wa watu hao.
Rosa Kornfeld-Matte, mtaalamu huru kuhusu masuala ya wazee kufurahia haki zote za binadamu ametoka wito huo wakati akikamilisha ziara yake ya kwanza rasmi nchini Georgia.
Nchi hiyo, kwa mujibu wa sensa ya watu iliyopita, inasemekana kuwa na idadi kubwa ya watu waliokula chumvi nyingi ,yaani wazee, katika eneo la Kaukasia kusini, ambapo ilionyesha kila mtu mmoja kati ya watano ana umri wa miaka 60 au zaidi. Taarifa inasema hii ina maanisha kuwa ifikapo mwaka wa 2050, asilimia ya waliona umri zaidi ya miaka 60 itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 30.
Kornfeld-Matte amesema kuna taarifa mbalimbali za unyanyasaji wa wazee ukifanywa na watu tofauti wakiwemo hata watu wa familia na wanaowahudumia.
Ameiomba serikali ya nchi hiyo kuja na mbinu mpya za kuzuia vitendo hivyo. Pia amekaribisha hatua ya serikali ya Georgia, ya hivi majuzi, ya kukubali mpango tekelezi wa kitaifa wa kufanikisha sera ya serikali kuhusu idadi ya watu wanaozeeka kama hatua moja iliokuwa inasubiriwa kwa hamu kuelekea kuboresha mfumo wa kuwasaidia wazee.
No comments
Post a Comment