Writen by
sadataley
7:50 PM
-
0
Comments
Baada ya kuwasili salama Algiers, Algeria, kikosi cha Taifa Stars kimeanza rasmi mazoezi jioni ya leo huku kukiwa na changamoto ya hali ya hewa.
Taarifa zinaleza wachezaji wamekuwa wakipatwa na wakati mgumu kutokana na hali ya hewa kuwa si rafiki kwao.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema kiwango cha baridi nchini humo ni nyuzi joto 7, kitu ambacho kinawaweka wachezaji katika wakati mgumu.
Stars imeanza mazoezi jioni ili kuzoea mazingira kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Algeria.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Stars ilifungwa na Algeria kwa jumla ya mabao 7-0
No comments
Post a Comment