Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, March 23, 2018

Serikali yawapiga marufuku Madaktari

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ni marufuku kwa madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa afya bila kupima wanafunzi husika iwapo ana ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB) au laa kwani kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

Pia amesema Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB na huku akieleza mpaka sasa takribani watoa huduma 1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu na hivyo wanaweza kuwabaini wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

Waziri Mwalimu ametoa kauli hiyo leo kwenye tamko lake   kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya TB duniani ambayo hufanyika Machi 24 ya kila mwaka ambapo amefafanua TB ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi duniani.

Hivyo amasema ili kukabiliana na ugonjwa huo pamoja na hatua mbalimbali zinazochukuliwa amewaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment