Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 22, 2018

Samatta aipongeza TFF kuchagua mchezo wa Stars dhidi ya Algeria



Kueleka mchezo wa kalenda ya FIFA ambao ni wa kirafiki kati ya Algeria dhidi ya Taifa Stars, Nahodha Mbwana Samatta amesema itakuwa ni kipimo kizuri.

Akizungumza na kituo cha Radio EFM kupitia kipindi cha Sports Headquarters, Samatta amesema analipongeza Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kuchagua mechi hiyo.

Samatta ameeleza mechi hiyo itakuwa ni kipimo kizuri kwao kutokana na utofauti wa viwango uliopo baina ya timu hizo mbili kutofautiana kwa mbali.

Ameongeza kwa kushauri ifikie hatua waendelee kutafuta timu ambazo zinakuwa bora dhidi yao ili waweze kupata nafasi nzuri ya kujipima, tofauti na wanapokutana na zenye viwango vidogo ambazo hata wakishinda hawapandi kwenye ubora wa soka duniani.

Katika ubora wa viwango vya soka duniani Tanzania imeshika nafasi ya 146 wakati Algeria ikiwa imeshika namba 60, Taifa Stars itacheza mchezo wa leo dhidi ya Algeria kuanzia majira ya saa mbili kamili usiku.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment