Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 24, 2018

Papa Francis aomba msamaha kwa mauaji Rwanda

Papa Francis akiwa na Rais Kagame Vatican

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPapa Francis akiwa na Rais Kagame Vatican
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa "dhambi na makosa yaliyotekelezwa na Kanisa na waumini wake … ambao walitekwa na chuki na ghasia" wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda.
Alikuwa akiongea baada ya kukutana na Rais Paul Kagame mjini Vatican.
Ombi lake la msahama limetokea baada ya ombi la Rwanda Novemba mwaka jana kwa Vatican kuomba radhi kutokana na mchango wa mapadri wa kanisa Katoliki na baadhi ya viongozi wake wakati wa mauaji hayo ya mwaka 1994.
Kwa mujibu wa Vatican Radio, Papa pia "ameelezea nia yake kwamba kutambua udhaifu huu wa kanisa kipindi hicho, ambao, uliathiri sana sifa za Kanisa, kunaweza kuchangia 'kutakaswa kwa kumbukumbu' na kuendeleza, kwa matumaini na uaminifu, amani siku za usoni."
Wakati wa mauaji hayo yaliyodumu siku 100, Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa kadiri waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo yalitekelezwa hadi katika makanisa ambapo watu walikuwa wamekimbilia kutafuta hifadhi.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment