Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 25, 2018

Naibu Waziri awataka wakandarasi wote wenye leseni kulipa kodi

NaibuWaziri wa Madini, Doto Biteko amesema madini ya ujenzi na viwanda yanaipatia serikali fedha nyingi kupita aina nyingine zote za madini yanayopatikana nchini.

Akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini mjini Dodoma jana akiwa kwenye ziara ya kazi, Biteko alisema, takwimu za makusanyo ya serikali zinabainisha hayo.

“Mfano mwaka 2016/17, takribani tani milioni 15.6 za madini ya ujenzi zilizochimbwa, zilizalisha shilingi bilioni 230.6; ambapo katika hiyo, ulipatikana mrabaha wa shilingi bilioni 7.1,” amesema Naibu Waziri.

Akifafanua zaidi, alieleza kuwa idadi ya wachimbaji wa dhahabu na madini mengine nchi nzima ikijumlishwa, haiwezi kufika hata robo ya wale wanaofanya shughuli za madini ya ujenzi nchini.

Alisema serikali imejipanga kuhakikisha inaongeza vituo vya madini ya ujenzi na viwanda kutoka 85 vilivyopo sasa nchi nzima hadi kufikia 174.

“Nina uhakika tukiviongeza vituo kufikia idadi hiyo, tutakusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi bilioni 15 katika madini hayo pekee,” alisema Biteko.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alitoa mwito kwa makandarasi wote wanaotekeleza miradi mbalimbali hususani ya ujenzi wa barabara kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuzingatia sheria ya madini inayomtaka kila mtu aliyepewa leseni kulipa tozo na kodi mbalimbali ambazo zimeelekezwa na sheria hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment