Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 29, 2018

IGP Sirro: "Hali ni shwari"

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Simon Sirro amesema ushirikiano unaoendelea kutolewa na wananchi kwa jeshi hilo, umesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa nchini na kuongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha Sikukuu ya Pasaka itasherehekewa kwa amani na utulivu

IGP Sirro ameyasema hayo ikiwa zimebaki siku chache kufika Sikukuu ya Pasaka na kuongeza kuwa kiujumla hali ya usalama ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa, wakati jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.

Ameongeza kwa kusema jeshi hilo linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.

Amewataka wazazi kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment