UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Friday, March 30, 2018

ASKOFU MALASUSA: MSIFANYE MAMBO KWA KUFUATA MAKUNDI


Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Askofu wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, amewataka waumini wa kanisa hilo kujipambanua kwa kufahamu mema na mabaya badala ya kufuata na kufanya mambo kwa kufuata kinachosemwa na makundi ya watu.
Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 30, katika Ibada takatifu ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front,  jijini Dar es Salaam.
Dk. Malasusa amesema hata kifo cha Yesu Kristo kilitokana na Pilato kusikiliza kundi kubwa la watu waliotaka asulubiwe.
“Watu wengi hufanya maamuzi kwa kufuata makundi ya watu yanasema nini, kwa hiyo hata kifo cha Yesu Kristo kiliharakishwa na kundi la watu waliopiga kelele asulubiwe na kuwachanganya viongozi.
“Hivyo ndivyo tunavyoishi leo kwa kufuata makundi ya watu, kwa hiyo lazima wakristo tujipambanue. Ijumaa Kuu ni zaidi ya kuvaa nguo nyeusi na kutokula baadhi ya chakula,” amesema Askofu Malasusa.
Mtanzania
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment