Kocha wa msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema kwamba, sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao
“Tunashukuru tumerudi salama, mechi yetu ilikuwa nzuri hatukutumia nguvu nyingi kwa sababu tulishinda 4-0 hapa ukizingatia tuna mechi za ligi kwa hiyo hatukutaka kujichosha sana, tulichohitaji ugenini ni kutoruhusu goli na sisi tupate angalau goli moja jambo ambalo tulifanikiwa.”
“Kwanza hatuangalii hata huo mchezo wetu na hiyo timu ya Misri, hapa mbele tuna mechi za ligi ambazo ni muhimu kuliko hata hiyo mechi na Al Masri.
“Tunaiandaa timu kwa ajili ya mechi dhidi ya mbao, hiyo Al Masri ukifikika wakati wake tutajiandaa.”
“Mechi dhidi ya mbao ni ngumu lakini ni lazima tushinde kwa sababu hakuna kingine tunachoweza kufanya kwa sababu tukitoka sare tunazidi kupoteza nafasi na sisi hatutaki kupoteza nafasi kwa sababu ndio nafasi pekee iliyobaki kwa Simba kushinda ubingwa.”
No comments
Post a Comment