Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 21, 2018

Messi afuta mkosi na Chelsea huku Bayern wakifanya kile walichofanya 1980


Kabla ya leo hii, Lionel Messi alikuwa hajawahi kuwafunga Chelsea katika michezo 8 iliyopita ambayo waliwahi kukutana, pamoja na mabao 595 aliyokuwa nayo hakukua na bao vs Chelsea.
Lakini usiku wa leo Lionel Messi amefuta mkosi huo baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea japo bao lake lilikuwa la kusawazisha baada ya Chelsea kutangulia kupitia Willian.
Bao la leo la Willian lilikuwa bao lake la 9 katika klabu bingwa Ulaya(muda wote) na sasa anakuwa amefunga mabao 6 kati ya hayo nje ya box huku Messi sasa anakuwa na jumla ya mabao 18 vs timu za Uingereza.
Bayern Munich wakiwa nyumbani walishusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Bestikas waliokuwa pungufu baada ya Domagoj Vida kupewa kadi nyekundu dakika ya 16 na kuwachapa bao 5 kwa nunge.
Mabao kutoka kwa Thomas Mueller(2), Roberto Lewandoski(2) na Kingsley Koman yanawafanya Bayern kufikia rekodi yao ya mwaka 1980 ya kucheza michezo 14 ya mashindano tofauti na kushinda yote mfululizo.

Shaffihdauda
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment