Kauli ya kocha wa Man City Pep Guardiola kuwa Man City hawawezi kutwaa mataji yote manne msimu huu, imedhihirika usiku wa February 19 2018 wakati wa game yao ya Kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic iliyochezwa katika uwanja wa The DW.
Pamoja na Man City kuwa mahiri katika hali ya umiliki wa mpira kwa dakika zote 90 wakimiliki kwa asilimia 83 kwa asilimia 17 dhidi ya Wigan Athletic, Man City wamekubali kipigo cha goli 1-0 lililofungwa dakika ya 80 na William Grigg.
Baada ya kufunga goli hili William Grigg kwa sasa anakuwa amefunga jumla ya magoli saba msimu huu katika Kombe la FA, hayo yakiwa ndio magoli mengi zaidi kufungwa na mchezaji mmoja katika Kombe la FA msimu huu.
No comments
Post a Comment