Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 20, 2018

Maelfu ya Wazimbabwe wauaga mwili wa 'Jenerali wa Watu' Tsvangirai; maziko yake kufanyika leo

Maelfu ya Wazimbabwe wauaga mwili wa 'Jenerali wa Watu' Tsvangirai; maziko yake kufanyika leo
Hayati Tsvangirai alifariki dunia Jumatano iliyopita ya tarehe 14 mwezi huu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi thakili ya saratani.
Hayati Morgan Tsvangirai, enzi za uhai wake
Kiongozi huyo wa upinzani, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 65 ametajwa kuwa ni 'Jenerali wa Watu' aliyewaongoza katika harakati raia masikini wa Zimbabwe, wafanyakazi wa vibarua na vijana tokea mwaka 1988.
Wakati wa uhai wake, hayati Morgan Tsvangirai pamoja na wafuasi wake walipigwa, walidhalilishwa na hata kutuhumiwa kwa mashtaka ya uhaini katika enzi za utawala wa Robert Mugabe.
Bi Chioniso Mazivanhanga, mama wa miaka 59 ambaye anasema alikuwa akimjua Morgan Tsvangirai tangu mwaka 1976 alipokuwa kiongozi wa jumuiya wa wachimba migodi, amemuomboleza mwanasiasa huyo kwa kusema: "Tsvangirai hakumbagua yeyote. Alimpenda kila mtu".
Rais Emmerson Mnangagwa, siku ya Jumapili alifika nyumbani kwa hayati Tsvangirai kutoa mkono wa pole na kuiahidi familia yake kuwa serikali italipia gharama zake zote za matibabu.
Akiongoza hafla ya kuuaga mwili wa kiongozi huyo wa MDC hapo jana, Mnangagwa amesema maziko yake yatapewa hadhi ya kitaifa kuenzi mchango wake katika kupigania amani na demokrasia. Viongozi wa vyama vya upinzani kutoka nchi kadhaa za Afrika pia walishiriki kwenye shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho kwa hayati Tsvangirai.
Maziko ya Morgan Tsvangirai yanafanyika leo kijijini kwao Buhera mahali alikozaliwa, yapata kilomita 200 kusini mashariki mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.
Parstoday.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment