Marehemu John Chipaka enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani nchini cha TADEA, John Lifa Chipaka amefariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Ibrahim Haji ya jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Marehemu Chipaka aliwahi kuwa Katibu wa ANC wakati wa kudai uhuru enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, pia aliwahi kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 na jina lake kukatwa na Tume ya Uchaguzi kwa kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Tutaendelea kuwajulisha taarifa zaidi kuhusu msiba huo.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
No comments
Post a Comment