Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, August 31, 2017

Rasmi Serikali yaanza kukabidhi leseni kwa machapisho.

Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.

Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema  utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.

“Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti  na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.

Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.

Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.

“Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.

“Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment