Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, August 1, 2017

Polisi watoa kibali rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda akamat

Polisi nchini Malawi wametoa kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani Joyce Banda kuhusiana na sakata ya ulaji rushwa inayofahamika sana kama Cashgate wakati wa utawala wake.

Polisi wamesema wamepata ushahidi wa kuaminika kuhusiana na sakata hiyo ya $250m (£190m).

Kashfa hiyo „inaibua uwezekano kwamba huenda rais huyo wa zamani alitenda makosa yanayohusiana na kutumia vibaya mamlaka na utakatishaji wa fedha."

Bi Banda yuko nje ya nchi na polisi wan chi hiyo wamesema wataomba msaada kutoka kwa polisi wa kimataifa Interpol kuhakikisha anarejea nchini humo kujibu mashtaka.

Cashgate ndiyo sakata kubwa zaidi ya ufisadi kuwahi kutokea katika historia ya Malawi.

Sakata hiyo inahusisha kuporwa kwa fedha za umma wakati wa utawala wa Bi Banda.

Rais huyo wa zamani hajazungumzia tuhuma hizo zilizotolewa dhidi yake.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment