Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club, Haji Sunday Manara aiomba Shirikisho la soka nchini (TFF) iwaruhusu kuchezesha wachezaji tisa uwanjani badala ya 11 katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga SC.
Manara ameyasemahayo huku akitanabaisha kuwa kipigo chao kwa Yanga hakiepukiki.
“Mchezo wa Yanga na Simba natamani uwekesho kwa sababu inasaidia kupunguza kelele mtaani na maneno ya kuzuazua”.
“Tunawaomba TFF kama wataweza waturuhusu tuanze na wachezaji tisa hivi kama wataturuhusu na kanuni zinaruhusu tutawaandikia barua rasmi ikiwezekana tuanze tisa tutawafunga tu Yanga”
Afisa huyo aliyetoka kifungoni hivi karibuni kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameongeza kuwa ameyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba Omog juu ya kumvua unahodha, Jonas Mkude
“Mimi ukiniambia, kwangu nimefurahia hili kwa sababu ukiwa nahodha unakuwa unabeba vichwa vya wachezaji kumi sasa kutolewa katika unahodha itamsaidia kumrudisha katika kiwango chake zaidi”.
No comments
Post a Comment