Writen by
sadataley
11:24 AM
-
0
Comments
Mahakama kuu nchini Kenya imepinga jaribio la kusistisha marufuku ya mifuko ya plastiki inayotarajiwa kutekelezwa siku ya Jumamosi.
Watengenezaji wa mifuko hiyo wanasema kuwa hatua hiyo itasababisha watu 8000 kupoteza kazi zao iwapo marufuku hiyo itatekelezwa.
Akitoa uamuzi huo mahakamani, jaji alisema kuwa kuondoa marufuku hiyo kutaathiri kwa kiasi kikubwa sheria za usimamizi wa mazingira huku akisisitiza kuwa uhifadhi wa mazingira ni muhimu kuliko maslahi ya kibiashara.
Watengenezaji wa mifuko ya plastiki pamoja na wafanyibiashara wa mifuko hiyo walienda mahakamani wakipinga ilani iliotolewa na serikali inayopinga utengenezaji na uagizaji wa mifuko ya plastiki kutoka nje.
Walidai kwamba serikali itawaachishwa kazi maelfu wa raia mbali na kuathiri uchumi wa taifa hilo.
Hili ni jaribio la tatu katika kipindi cha miaka kumi kwamba Kenya imejaribu kupiga marufuku mifuko ya plastiki.
Wizara ya mazingira inasema kuwa mtu yeyote atayepatikana akitengeza ama kufanya biashara ya mifuko ya plastiki atahudumia kifungo kisichopungua mwaka mmoja ama faini isiopungua dola 19, 000 za Marekani.
Kenya itajiunga na mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga marufuku mifuko ya plastiki ikiwemo Rwanda na Eritrea.
BBC
No comments
Post a Comment