Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 27, 2017

KRC Genk yaua 1-0, Samatta atokea benchi

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana aalicheza kwa dakika saba baada ya kutokea benchi, timu yake, KRC Genk ikishinda 1-0 nyumbani dhidi ya Mechelen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena, Genk.

Samatta aliingia dakika ya 83 kuchukua nafasi ya mshambuliaji kinda wa miaka 21, Mdenmark, Marcus Ingvartsen katika mchezo ambao bao pekee la ushindi la Genk lilifungwa na kiungo kutoka Hispania, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 38.


Huo unakuwa mchezo wa 60 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 35 alianza na mechi 22 ametokea benchi.

Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 21.

Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Vukovic, Uronen, Colley, Brabec, Mata, Berge, Malinovskyi/Heynen dk86, Pozuelo/Aidoo dk91, Writers, Buffalo na Ingvartsen/Samatta dk83.

KV Mechelen: Coosemans, Vitas, Matthys, Croizet, Zipper, Cocalic/The White dk78, Schoofs, Cobbaut, Filipovic/Kawaya dk68, Rherras/Claes dk68 na Drazic.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment