Writen by
sadataley
10:05 AM
-
0
Comments
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, viongozi wa upinzani sio maadui wa serikali hivyo kuna haja ya kushirikiana nao.
Tundu Lissu, mmoja wa viongozi wa upinzani nchini Tanzania ambaye pia ni mwanasheria
Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi na vyama tawala barani Afrika kutowachukulia viongozi wa upinzani kuwa maadui na badala yake kuwafanya kuwa washirika wakuu.
Kikwete amesema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Afrika kuhusu uongozi bora na sheria uliofanyika mjini Johannesburg ambapo alitoa changamoto kwa vyama vya kisiasa barani Afrika kushirikiana.
Rais mstaafu wa Tanzania amebainisha kuwa, badala ya kuuchukulia upinzani kuwa adui, viongozi na vyama vilivyoko madarakiani vinapaswa kuwachukulia wapinzani na vyama vya upinzani kwamba, ni washirika katika kuimarisha demokrasia inayoheshimu sheria.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wito huo wa Jakaya Kikwete umepongezwa na wasomi na wanaharakati mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Onesmus Ole Ngurumwa Mkurugenzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) amesema kuwa taarifa ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete ni funzo kubwa kwa wanasiasa barani Afrika na hususan Tanzania.
Mwanaharakati huyo wa masuala ya haki za binadamu ammewataka viongozi wa zamani kujitokeza hadharani na kuliangazia tatizo hilo huku akiwashauri wapinzani kutoogopa kufanya mazungumzo na Rais Magufuli ili kutafuta suluhu ya kudumu.
Aidha amesema kuwa, Kenya ni mfano mzuri kwetu katika eneo hili. Upinzani unatumia uhuru wa kidemokrasia na hali hiyo imesaidia kuondoa hali ya wasiwasi mbali na kuimarisha maendeleo.
Parstoday
No comments
Post a Comment