Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 14, 2017

Zaidi ya abiria 400 waahirisha safari baada ya meli kuzuiwa

Zaidi ya abiria 400 waliokuwa wakitarajia kusafiri kuelekea katika Kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza, wamejikuta wakiahirisha safari baada ya Mamlaka ya vyombo vya usafiri wa nchi kavu na Majini nchini (Sumatra), kuizuia Meli ya M.v Nyehunge isiendelee na safari zake.

Wakizungumza na Channel Ten Jijini Mwanza, baadhi ya abiria wamesema kitendo cha Meli hiyo kuzuiwa kutoendelea na safari zake, kimewaweka kwenye wakati mgumu, kutokana na kisiwa hicho kwa sasa kutokuwa na Meli yoyote inayotoa huduma.

Abiria hao wamejikuta wakikabiliwa na adha hiyo bila kufahamu hatma ya usafiri mbadala kwa sasa, baada ya meli nyingine ya Serikali ya Mv. Crarias kusimamishwa kwa ajili ya matengenezo.

Kutokana na adha hiyo Channel imebisha hodi katika Ofisi za (Sumatra) Mkoa wa Mwanza, ili kufahamu sababu za meli hiyo kusimamishwa, ambapo afisa mwandamizi wa Mamlaka hiyo Iroga Nashon, akaeleza sababu zinazodaiwa kuisimamisha Meli hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment