Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum anaratajiwa kuwa mgeni rasimi kesho katika ufungaji wa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) ilisema kuwa maonesho hayo yataitimishwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Salum ambaye atatoa vyeti kwa washindi wa mabanda bora yaliyoshiriki maonesho hayo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa maonesho hayo yatafungwa majira ya saa saba kwa hotoba ya Waziri huyo na kufuatana na viongozi mbalimbali wakiwemo waandaji wa Maonesho hayo.
Wakati huo katika maonesho hayo wananchi wameendelea kufika katika viwanja vya sabasaba kwa kupata huduma pamoja bidhaa za washiriki.
Mabanda ambayo yamekuwa na watu katika siku ya maonesho tangu siku kwanza hadi leo ni mabanda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
No comments
Post a Comment