Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 14, 2017

Wamiliki wa mabasi wapigwa mkwara mzito

MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imetangaza kuwafikisha mahakamani wahudumu wa mabasi watakaobainika kutoza wananchi viwango vikubwa vya nauli tofauti na maelekezo ya Sumatra.

Pia imewataka wamiliki wa magari ya abiria mkoani hapa, kuyapeleka magari hayo Veta kwa ajili ya kuandikwa ubavuni viwango vya nauli wanavyotakiwa kutoza kwa wasafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Dk. Walukani Luhamba. Alisema wamiliki hao wamepewa wiki mbili kuhakikisha wanakamilisha agizo hilo na kwamba baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayeshindwa kutekeleza maelekezo hayo.

Dk. Luhamba alisema mamlaka hiyo imeamua kubandika viwango vya nauli kwenye ubavu wa mabasi ili  abiria wafahamu viwango vya fedha wanavyotakiwa kulipa ili wanapozidishiwa watoe taarifa Sumatra kwa hatua zaidi.

Alieleza wameamua kuchukua hatua hiyo  kutokana na baadhi ya wahudumu wa mabasi kutokuwa  waaminifu  kwa  kuwatoza wananchi nauli za juu na kwamba wanatumia uelewa mdogo wa  abiria kutofahamu viwango wanavyotakiwa kulipa kwa safari.

“Tutawafikisha mahakamani wenye mabasi watakaotoza nauli kinyume na tangazo lililotolewa na serikali, watakaoshikwa na kufikishwa kwenye sheria  watatozwa  faini ya Sh. 300,000 au kifungo cha mwaka mmoja jela” alisema.

Kuhusu kuandikwa ubavuni mwa magari hayo viwango vya nauli, alisema hiyo ni moja ya mpango kazi wa kudhibiti kupanda holela kwa nauli kunakofanywa na wahudumu na wamiliki wa mabasi.

Pia alisema hatua hiyo na itawawezesha wananchi kulalamika anapotozwa zaidi na kuwataka  makondakta wanapochukua pesa ni lazima kutoa tiketi na si lazima wangoje kudaiwa na abiria.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment