Naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi anasema kuwa, vikwazo vipya vya kiuchumi vilivyotolewa na Marekani, vitahujumu uhusiano bora ulipo kati ya Moscow na Washington.
Sergei Ryabkov amesema kuwa utayumbisha kabisa uhusiano wao.
Awali, baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kwa kauli moja kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini.
Urusi inaadhibiwa kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani, huku Korea Kaskazini na Iran wakiadhibiwa kutokana na mipango yao ya kufanyia majaribio zana zao za makombora ya kinuklea.
Mswaada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti, kabla ya kupelekwa kwa Rais Donald Trump ili audhinishe na kuwa sheria kamili.
No comments
Post a Comment