Kuoa au kuoelwa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha.
Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kutokuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana.
Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa.
1. Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii.Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine.
Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani, kikapanda kikashuka.
Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao au kutazama Tv zaidi ya kuanza kuiga yale aliyoyaona. Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii hakumbuki hata kufanya usafi ndani.
2. Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani.Wanawake wengi wa ki-Afrika kwa vile wamekwenda shule wakatambua mambo ya haki sawa kwa wote na wengine kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.
Kutokana na hali hii, wanawake wamekua wakujiremba tangu mawio hadi machweo, ukitazama kucha zao zilivyondefu unajiuliza huyu anafua kweli?
Wengine wameamua kuajiri watu wa kuwafulia hadi nguo za ndani. Kwa hali hii usitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.
3. Kujipodoa hadi sura yako ya asili inasahaulika.Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza. Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.
Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio-serious kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuta. Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiyejiremba (wenyewe huita natural)
Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa.
No comments
Post a Comment