Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 22, 2017

Singida United yaibomoa Yanga

Klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu imemaliza usajili wake kwa kuibomoa klabu ya Yanga baada ya kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke.

Aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi na kocha wa zamani wa Yanga , Hans Pluijm ambaye sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Singida United alisema kuwa katika klabu yake hiyo alikuwa amebakiwa na nafasi moja ili kujenga kikosi chake vizuri, nafasi hiyo ambayo imejazwa na Kaseke.

Mkurugenzi wa Singida United Bw. Festo R. Sanga amethibitisha kuchukuliwa kwa Deus Kaseke katika klabu yake hiyo na kusema amesaini mkataba wa miaka miwili.

"Hatimaye Deus David Kaseke anaswa na Singida United, amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia timu yetu na tayari anaelekea Mwanza kuungana na wenzake" alisema Festo Sanga

Timu ya Singida United itakutana na klabu ya Yanga katika mchezo wa kirafiki ambao utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5/08/2017 uwanja wa Taifa.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment