Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, July 30, 2017

Simanjiro: Migodi miwili yafungiwa

Sakata la kifo cha mchimbaji madini ya Tanzanite katika Mgodi wa Gem & Rock Venture wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, limechukua sura mpya baada ya mgodi huo na ule wa CT kufungiwa.

Takribani kwa siku tano mfululizo kulikuwa na vurugu zilizotokea kwenye migodi hiyo iliyopakana huku kila upande ukituhumu mgodi mwingine kuwa unawarushia mabomu ya kutengeneza kienyeji.

Kutokana na vurugu hizo mchimbaji wa mgodi wa Gem & Rock Venture, Lembris Mbatia (22) alifariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa bomu la kutengeneza kienyeji na kulipuliwa mgodini humo na wafanyakazi wa Kampuni ya TanzaniteOne.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma amesema amesitisha shughuli za uchimbaji kwenye migodi hiyo miwili ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya mgogoro uliopo sasa.

Juma amesema wameamua kusitisha kwa muda shughuli za uchimbaji madini kwenye migodi hiyo miwili ili yafanyike mazungumzo baina ya pande hizo mbili na hatimaye kupata mwafaka wa uchimbaji salama.

Amesema wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini, kutoka kitengo cha ukaguzi wa migodi wanatarajia kufika eneo hilo na kukagua migodi hiyo miwili kwa lengo la kupata suluhu.

Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Zephania Chaula alizitaka pande hizo mbili kukaa pamoja ili kupata suluhu ya mgogoro uliosababisha kifo cha mchimbaji mmoja na wengine kujeruhiwa.

"Pamoja na hayo, bado nasisitiza kutotumika kwa matumizi ya mabomu ya kutengeneza kienyeji, nimeshaagiza polisi wawachukulie hatua kali  wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu," amesema Mhandisi Chaula.

Mwananchi:
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment