Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 19, 2017

Raisi Magufuli atoa msaada Mtwara

Rais Dk. John Pombe Magufuli ametoa msaada wa vitanda 20,magodoro 20 pamoja na mashuka 50 kwa hospitali ya Mkoamaindo iliyopo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha wananchi anaowaongoza wanapata huduma bora za afya.

Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 kwa niaba ya Rais Magufuli,mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amesema kuwa Rais Magufuli ametoa msaada huo wa vitanda,magodoro pamoja na mashuka ili wananchi wake wapate huduma bora za afya jitihada ambazo anazifanya nchi nzima.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Masasi Dk. Mussa Rashid ambae amepokea msaada huo amesema kuwa msaada huo umesaidi kupunguza tatizo la ukosefu wa vitanda vya kulaza wagonjwa katika hospitali ya mkomaindo.

Dk. MUSSA RASHID-Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Masasi.

Aidha makabidhiano hayo yameenda sambamba na makabidhiano ya kadi za uanachama wa CHF kwa wazee wa wa kata ya Temeke ,makabidhiano ambayo yamefanyika katika ujenzi wa zahanati ya kata ya temeke inayokusudia kuondoa adha ya wakazi zaidi ya elf 11 wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment