Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 21, 2017

Rais Magufuli asitisha kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba kusimamisha kuwapa uraia raia wa Burundi kuanzia sasa.

Akizungumza  leo, Alhamisi Julai  20 wakati wa ziara yake mkoani Kagera, akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alimtaka asiwape uraia  wanaotoka nchi nyingine.

“Rais amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka kwenu,” amesema.

Awali, Rais Nkurunziza amezungumza na wananchi hao na kuwataka raia wa Burundi warudi nchini mwao kwani kwa sasa amani imerejea.

 Kadhalika, Waziri Nchemba amesema katika kipindi cha 2016/17, Tanzania imewapa uraia wakimbizi wa Burundi 1060.

 Pia, Waziri Nchemba amesema kati ya wakimbizi 247,000 waliopo nchini, 5,000 wameomba kurudi kwao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment