Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 21, 2017

Mtoto na mkwe wa Rais Trump, waitwa kuhojiwa na tume ya uchunguzi ya bunge la seneti Marekani

Tume ya uchunguzi katika Bunge la Seneti nchini Marekani, imewaita watu watatu wa karibu na Rais Donald Trump wa nchi hiyo kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya uhusiano wao na serikali ya Russia.
Donald Trump Jr, mwana wa Rais Donald Trump wa Marekani
Natalia Veselnitskaya, wakili wa Russia anayetajwa kufanya mawasiliano na Donald Trump Jr
Donald Trump Jr, mtoto wa kiume wa Trump, Jared Kushner, aliyemuoa binti yake na rais huyo na Paul Manafort mmoja wa watu wa karibu na Trump, ni shakhsia waliotakiwa kufika na kutoa maelezo mbele ya tume hiyo juu ya kuwa na mahusiano na Russia.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Paul Manafort na Donald Trump Jr watatoa maelezo yao mbele ya tume hiyo hapo tarehe 26 ya mwezi huu kuhusiana na kadhia hiyo. Barua pepe za mwana huyo wa Trump zinaonyesha kwamba, mwanzoni mwa mwezi huu alifanya mawasiliano na Natalia Veselnitskaya, mwanasheria na wakili wa Russia akitaka kupata ripoti juu ya Bi Hillary Clinton, aliyekuwa hasimu wa baba yake katika uchaguzi wa rais wa mwaka jana 2016, kwa lengo la kutaka kumchafua mwanamama huyo.
Wakati huo huo, Jared Kushner mume wa Ivanka Trump, binti ya rais huyo wa Marekani, ametakiwa naye kuwasili mbele ya tume hiyo ya uchunguzi hapo tarehe 24 kujibu tuhuma zinazomkabili za kuwa na mahusiano na serikali ya Russia. 
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment