Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 18, 2017

Matawi sita ya ANC yamteuwa Sisulu kuongoza chama tawala

Lindiwe Sisulu Waziri wa Maendeleo ya Makazi wa Afrika Kusini amekubali uteuzi wa matawi sita ya chama tawala nchini humo ANC ambayo yamemteuwa kuongoza chama hicho.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini  
Bi Sisulu ambaye ni waziri aliyehudumu kwa muda mrefu na anayetoka katika familia ambayo pamoja na Mandela walifahamika kama shakhsia mashuhuri katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini (Apartheid), hivi sasa amejiunga katika mchuano mkali wa kuwania kiti cha uongozi wa ANC kinachoshikiliwa na Rais Jacob Zuma anayekabiliwa na kashfa ya ufisadi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.
Matawi ya ANC yasiyopungua sita yamemteuwa Sisulu kuwa kiongozi wa chama hicho na yeye amekubali uteuzi huo hadharani.  Akizungumza na televisheni ya eNCA, Bi Lindiwe Sisulu amesema kuwa ana kibarua kigumu mbele yake ili kukirejeshea heshima na hadhi chama tawala cha ANC na kukihakikishia ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019. 
Parstoday 
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment