Marekani imesema kuwa kuwa imefanikiwa kuufanyia majaribio mtambo wake wa kujikinga dhidi ya makombora, na kurusha ndege zake aina ya B-1 bomber katika rasi ya Korea.
Zoezi hilo ni jibu la moja kwa moja kwa majiribi ya hivi punde ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Kombora lililofyatuliwa na jeshi la wanahewa la Marekani katika anga za bahari ya Pacific liliharibiwa na kombora la Thaad.
Ndege za Marekani za B-1 bombers pia zilifanya mazoezi katika eneo la rasi ya Korea zikishirikisha ndege za Korea Kusini na Japan.
Siku ya Ijumaa Korea Kusini ilifanya jaribio la pili la kombora la masafa marefu ICMB ambalo ilisema kuwa linaweza kushambulia Marekani.
Jaribio hilo lilifanyika majuma matatu baada ya lile la kwanza la masafa marefu.
Siku ya Jumamosi rais wa Marekani Donald Trump aliilaumu China kwa kutoidhibiti Korea Kaskazini katika mipango yake ya nuklia kwa kufanya biashara ya mabilioni ya dola na Korea Kaskazizi.
No comments
Post a Comment