Rais John Magufuli amepeleka neema kwa wananchi wanaoshiriki maonyesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba baada ya kupendekeza kuongezwa kwa siku tano zaidi.
Maonyesho hayo yaliyoanza rasmi Juni 28 na kutarajiwa kumalizika Julai 8, sasa yatamalizika Julai 13, mwaka huu na kutimiza siku 16.
Akifungua maonyesho hayo jana, Jumamosi, jijini hapa, Rais Magufuli alimwomba Mwenyekiti wa Bodi ya Biashara (Tantrade) afikirie kuongeza siku ili wananchi waweze kushiriki kwa muda mrefu zaidi.
“Kama likiwagusa, waongezeeni muda wananchi washiriki kwa muda mrefu zaidi, muwape nafasi taasisi za kujifunza zaidi,” alisema na kuongeza:
“Ni siku muhimu sana katika maendeleo ya Tanzania, haya ni maonyesho yangu ya kwanza kama mualikwa, mwaka jana mgeni rasmi alikuwa mwingine mimi nilikuwa msindikizaji.”
Kutokana na pendekezo hilo la Rais, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Christopher Chiza alitangaza kuongeza siku tano baada ya Julai 8 siku maonyesho yatakapofikia kikomo.
No comments
Post a Comment