Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, July 26, 2017

Korea Kaskazini: Kutokuwa na umuhimu Marekani kuwapiga marufuku raia wake kuja kwetu

  • Shirika la ustawi wa kieneo la Wonsan Zone Development Corporation la Korea
  • Kaskazini limetangaza kuwa, marufuku iliyotangazwa na Marekani ya kuwazuia raia 
  • wake kufanya safari nchini humo, haitakuwa na taathira yoyote kwenye sekta ya utalii.
Wonsan limeongeza kuwa, Pyongyang inaiona marufuku hiyo kama isiyokuwa na umuhimu wowote. Msemaji wa shirika hilo Han Chol-Su ameitaja hatua hiyo ya Washington kuwa iliyosukumwa na siasa na kuongeza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Pyongyang havina taathira yoyote na kwamba Korea Kaskazini itaendelea kuimarisha harakati zake za makombora na silaha za nyuklia.
Shirika la Wonsan Zone Development Corporation ni moja ya mashirika makubwa yanayojishughulisha na sekta ya utalii nchini Korea Kaskazini. Ijumaa iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza rasmi hatua ya kuwapiga marufuku raia wake kufanya safari kwenda Korea Kaskazini. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, karibu watalii 5000 kutoka nchi za Magharibi hufanya safari kwenda Korea Kaskazini kila mwaka ambapo kati yao 1000 hutoka Marekani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imewaonya raia wake kufanya safari kwenda nchi hiyo ya Asia kutokana na hatari ya kutiwa mbaroni na serikali ya Pyongyang. Hii ni katika hali ambayo Pyongyang inasisitiza kuwa, inawatia mbaroni majasusi tu na sio raia wa kawaida.
Katika hatua nyingine Oleg Burmistrov, naibu wa timu ya mazungumzo ya nyuklia kutoka nchini Russia amefanya mazungumzo na Sin Hong-chol, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini juu ya njia za utatuzi wa mgogoro wa eneo la Korea. Katika mazungumzo hayo, Hong-chol  amesema kuwa ikiwa Marekani itaendeleza siasa zake za uhasama na vitisho dhidi ya Pyongyang, basi Korea Kaskazini haitorudi nyuma hata kidogo katika kujiimarisha kwa silaha za nyuklia na makombora ya balestiki. Oleg Burmistrovamesema kuwa ameshuhudia mkwamo mgumu wa kisiasa juu ya suala la utatuzi wa mgogoro wa eneo la Korea. Burmistrov aliyewasili mjini Pyongyang siku ya Jumamosi, aliondoka mjini hapo jana usiku.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment