Writen by
sadataley
7:56 AM
-
0
Comments
Na Salesi Malula
Kanisa la Tanzania Assemblies of God linaloongozwa na Askofu Mkuu wake Dk Barnabas Mtokambali limeandaa mechi kabambe ya mpira wa miguu kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kati ya timu ya Yanga Juniour na Halelujah kutoka Korea linalotarajia kufanyika katika uwanja wa taifa wa uhuru Jumamosi wiki hii.
Akiongea na Mtandao huu mchungaji kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Mbezi A Dk Huruma Nkone amesema kuwa wameamua kuwapa burudani ya kipekee watu wote bila kujali utofauti wa madhehebu yao na kuwaunganisha kushuhudia burudani ya kipekee ya mpira wa miguu ambayo inawauganisha watu wote bila kujali Imani zao.
Alisema maandalizi ya pambano hilo la kirafiki yamekamilika hakuna kiingilio chochote katika mechi hiyo itakayoanza muda wa saa nane mchana katika uwanja wa uhuru ambapo pia kutakua na program mbalimbali zitakazokua zikiendelea katika viwanja hivyo.
Akifafanua alisema mbali na mpira wa miguu pia kutakua na program mbalimbali za watoto ikiwepo michezo hivyo natoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto wao kuja kufurahia burudani mbalimbali zitakazokuwepo katika viwanja hivyo.
Pia kutakuwepo na burudani mbalimbali za nyimbo mbalimbali za kumtukuza Mungu kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwepo dansi maalum kutoka kwa waimbaji kutoka nchini Korea.
Kuhusiana na masuala ya ticketi kanisa linapenda kuwa taarifu wananchi wote kwenda kwenye kanisa lolote la Tanzania Assemblies of God na kupewa ticketi hizo bure na wengine wanaweza kupewa ticketi zao siku hiyo mlangoni mwa uwanja wa uhuru.
Akieleza lengo la mechi hiyo Dk Nkone amesema ni kudumisha umoja mshikamano na upendo kati ya nchi ya Korea na Tanzania na kuwapa burudani wananchi .
Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia yangaJ ounior itakapokua ikichua na timu ya hallelujah kutoka nchini korea na kushiriki katika michezo mingine itakayokua ikiendelea katika viwanja hivyo hii si ya kukosa alisisitiza.
No comments
Post a Comment