UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Tuesday, July 4, 2017

John Bocco aitwa Afrika Kusini kujiunga na Taifa Stars

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco ametua nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo nchini humo kutokana na mchezaji Mbaraka Yusuph kuwa majeruhi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ambapo amesema Bocco ameondoka jana nchini kuwafuata wenzake walioko huko kwa lengo la kuchukua nafasi ya mshambuliaji huyo mpya kutoka Azam Fc.

“Mbaraka amepata matatizo kule Afrika Kusini, hali ya hewa ya baridi imemletea matatizo ambayo kwa sasa yanamzuia kucheza hivyo wakati tunatazama hali yake tumemuita Bocco kwanza kuchukua nafasi,” alisema Madadi.

Taifa Stars itashuka dimbani kwa mara nyingine siku ya Jumatano dhidi ya Zambia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea kuchezwa huko Afrika Kusini baada ya kuichakaza bao 1-0 Bafana Bafana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment